Burudani

Dully Sykes: ‘Hakuna rapper wa Bongo anayefikia utajiri wangu’, Fid amjibu

Msanii mkongwe wa muziki nchini, Prince Dully Sykes amefunguka kuwa hakuna msanii wa Hip Hop hapa Tanzania anayemfikia kwa maendeleleo.

10601811_510475949098767_362612024_n

Dully ambaye anamiliki studio pamoja na vifaa vya muziki aliongea hayo mbele ya Fid Q.

“Kwa hapa nilipofikia na uwezo na mali nilizokuwa nazo hakuna mwana hip hop anayenifikia. Umaskini mliokuwa nao ni mwana hip hop gani anaweza akafikia uwezo wangu? Sio studio tu kwani mali ni studio peke yake!Katika mali zangu studio haipo, mimi ni mwanamuziki lakini wanahiphop ni maskini zaidi yangu mimi, siwezi taja mali zangu, kuna studio na home studio, wewe (Fid Q) una home studio,” alisema Dully kwenye maongezi ya kwenye basi la ziara ya Fiesta ambayo yalikuwa on the record (ruhusa kurekodiwa).

Baada ya kauli hiyo, Fid Q ameiambia Bongo5 kuwa Dully hajui utajiri anaouzungumzia huku akidai kuwa wasanii wa muziki wa kuimba wanapewa nafasi kubwa kwenye muziki wao na ndio maana wanakuwa na kiburi.

“Kwanza Dully ana utajiri gani kuliko wasanii wa Hip Hop? Mimi naona yupo kawaida sana. Sema wasanii wengi wa muziki wa kuimba wanapewa nafasi nyingi za kuonekana kuliko wana Hip Hop lakini sio kusema anawazidi utajiri,” alisema Fid Q.

Unahisi Dully ameongea ukweli? Funguka.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents