Burudani

Dudubaya awaota Godfather, Ogopa na Nisher

Dudubaya amesema anafikiria kushoot video ya wimbo wake wa ‘Kokoliko’ na director mmoja kati Godfather, Ogopa Deejays na Nisher.

dudu-baya

Akizungumza na Bongo5, Dudubaya amesema wimbo huo unahitaji director aliyetulia na mwenye creativity ya juu.

“Nimefikiria kufanya video ya Kokoliko na directors wenye uwezo na kipaji kwa sasa na niliowafikiria ni Godfather, Ogopa Deejays na Nisher. Ukiangalia kwa sasa hawa ni moja kati ya madirector wanaofanya vizuri kwenye video zao na wametengeneza base kubwa,” alisema Dudubaya.

Aliendelea kwa kusema, “Ukiangalia wimbo wa Kokoliko ni wimbo wa dance unahitaji creativity ya hali ya juu na hawa madirector niliowafikiria kufanya nao kazi najua wataweza,” aliongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents