Burudani

Dudu Baya: Sijaona nchi yenye wana Hip Hop fake kama Tanzania

Msanii mkongwe wa Hip Hop nchini, Godfrey Tumaini aka Dudu Baya amedai kuwa amezunguka katika nchini kibao duniani lakini hajawahi kuona nchi yenye wasanii wa Hip Hop fake kama wa Tanzania.

Dudu Baya alikuwa kama surprise kwa mashabiki wa Tabora

Akizungumza na Bongo5 jana, Dudu amesema aliwahi kujaribu kukutana na baadhi ya wasanii wa Hip Hop na kujadili baadhi ya changamoto zao ila ziligonga ukuta kutokana na uoga wao.

“Nimezunguka dunia nzima sijaona nchi yenye wana Hip Hop fake kama Tanzania,” amesema Dudu. “Yaani wana Hip Hop wa Tanzania ni fake, yaani hawajui maaana ya Hip Hop. Nilishawatafuta wengi tufanye harakati za kuokoa muziki wetu lakini nikiwafuata wanasema ‘aise bro hizi harakati ni ngumu’. Kama utakuwa unaona hata kutafuta haki yako ni ngumu utakufa ukiwa masikini kutokana na dosari za uzembe. Wewe unatakiwa uitetee jamii halafu unaogopa watu kwanini sasa uitwe mwana Hip Hop? Nilishawafuata wasinii wengi wa Hip Hop tutengeneze structure ya muziki wetu kibiashara lakini hawaeleweki. Nilishamfuata Professor, nilishakaa na Mwana FA, na nimeshakaa na wasanii wote wa Hip Hop unaowajua lakini wananiambia ‘bro hizi harakati zako hatuziwezi’,” amesema rapper huyo.

Katika hatua nyingine Dudu Baya amewataka wanawake wote ambao ni wadau kwenye burudani kuwasaidia wasanii wa kike wanaohitaji msaada.

“Unajua wanawake wanateseka sana kwenye hizi harakati za muziki wetu, tunahitaji kuwasaidia, kwa sababu presenter ili aicheze ngoma yake anahitaji kutoa rushwa ya ngono, producer pia, waandishi. Kwahiyo kiukweli wasanii wa kike wanahitaji kusaidiwa na wadau wa kike ambao wapo kwenye huu mtandao wa muziki. Kuna watangazaji kama akina DJ Fetty wapo wengi. Hao ndo wanatakiwa kuanzisha harakati za kuwasaidia wasanii wa kike. Nipo kwenye mchakato wa kuzungumza na baadhi ya wadau ili tujue tunajadili vipi ili kuwasaidia hawa ndugu zetu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents