Burudani

Dudu Baya anakuja na ‘Naibaka Dar Tour’

Msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop, Dudu Baya aka Mamba anajipanga kuja na tour yake ya muziki ambayo amepachika jina la ‘Naibaka Dar Tour’.
Dudu Baya

Akizungumza na Bongo5 Alhamisi hii, Dudu Baya amesema ameanzisha tour hiyo baada ya kuona mapokezi makubwa katika show yake iliyofanyika Maisha Club weekend iliyopita.

“Nimegundua naweza kutengeza pesa nyingi, show yangu ya Maisha imenifanya nianzishe tour ambayo nimeipa jina ‘Naibaka Dar Tour’,” alisema Dudu. “kwa mfano wiki ijayo tarehe 4 kuna tamasha la Komaa Concert2016 pale Kijitonyama Viwanja vya Posta, siyo tamasha langu lakini mimi ‘Nitaibaka Dar’, ni kama sehemu ya Naibaka Dar Tour,”

Aliongeza, “Lakini pia mimi binafsi nitakuwa na tour ambayo itaitwa ‘Naibaka Dar Tour’ ambayo labda nitakuwa mimi mwenyewe au nikisindikizwa na wasanii wachache, nitaandaa show mbalimbali hapa Dar es salaam na baadae hata nje ya Dar es salaam kwa sababu hii ni biashara,”

Kwa sasa Dudu Baya anafanya poa na wimbo wake ‘Kokoriko’ ambao ulitoka mapema mwaka huu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents