Picha

Drama baada ya kifo cha Goldie yaendelea, mwanamke aitwaye Ifeoma Harvey aibuka na kudai Goldie alimuibia mume!

goldie-wed-3

Drama baada ya kifo cha Goldie imeendelea kuchukua sura mpya na sasa mwanamke aitwae Ifeoma Harvey ameibuka na kudai kuwa Goldie Harvey alimuibia mume wake (Andrew Harvey)!

Ifeoma ametumia mtandao wa Facebook kusimulia upande wake wa story na kudai kuwa yeye Goldie walikuwa marafiki miaka ya nyuma. Kwa mujibu wa Ifeoma, Goldie alisubiri muda muafaka na kumnyakua Andrew Harvey nchini Nigeria, wakati alikuwa amemuoa Ifeoma.

“Hakujua kama siku moja kifo kitamuita ,” anasema Ifeoma, “Alimchukulia mwanaume huyo kila kitu na sasa Andrew Harvey amelazwa hospitali Malaysia.”

Aliendelea:

“Goldie alienda Malaysia kumsalimia mwanaume huyo mgonjwa kabla ya kwenda Marekani kuhuhudhuria tuzo za Grammy na kurejea kukutana na kifo chake kisichoeleweka. Goldie ni muongo, pretender na mhalifu. Anataka kupata fedha na umaarufu kwa gharama yoyote… amelazimisha muziki wake kama takataka kwenye vinywa vyetu, alienda BBA na kumess up na Prezzo… mwanamke aliyeolewa kabisa. Kwanini Andrew anapost picha za ndoa yao sasa hivi? Labda dawa aliyotumia imeisha machoni mwake (Andrew)! Andrew aufunge mdomo wake na aombe apone haraka kutoka kwenye kitanda cha hospitali Malaysia. Baada ya hapo anaweza kurudi London na kumuomba mke wake na watoto wake msamaha.”

Kupitia Facebook naye Andrew aliamua kukanusha madai ya Ifeoma kuwa amelazwa nchini Malayisia kwa kuandika:

HARVEY-FB-POST-11

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents