Burudani

Drake na Rihanna warudiana? waonekana night club pamoja

Drake na Rihanna wameanza kuonekana tena pamoja baada ya wawili hao kusemekana kutibuana na kila mmoja kuchukua hamsini zake siku za karibuni.

drake-rihanna-club

Rihanna na Drake wameonekana kwenye club moja iitwayo Griffin nightclub iliyoko New York Jumatatu usiku, na kuamsha hisia za watu wengi kuwa kuna uwezekano mapenzi yao yamerudi.

Inadaiwa kuwa Riri na Drizzy waliingia club kwa kupishana dakika 10, na walikaa club masaa mawili kabla ya kuondoka kwa kupishana dakika 21.

Kwa mujibu wa TMZ, chanzo kilichokuwepo ndani ya club hiyo kimedai walikaa karibu na muda mwingi walikuwa wakizungumza, wakitaniana na wakinong’onezana masikioni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents