Burudani

Drake, Kanye West na Justin Bieber wapanga kuzisusia tuzo za Grammy

Drake, Kanye West na Justin Bieber ni miongoni mwa mastaa ambao hawataudhuria katika tuzo za Grammy zinazotarajia kufanyika Jumapili ya Februari 12, 2017 katika ukumbi wa Staples Center uliopo mjini Los Angeles.

Drake ambaye amewekwa katika vipengele nane vya tuzo hizo, amedai hatohudhuria tuzo hizo kutokana na kuwa na ziara yake katika bara la Ulaya ambayo imeingiliana na siku ya utoaji wa tuzo hizo.

Naye Kanye ambaye anawania tuzo nane katika tuzo hizo ameamua kutohudhuria kutokana na tuzo hizo kuonekana kuwa za kibaguzi kwakuwa mara kibao amekuwa akishindwa kupata tuzo hizo pale anapokuwa amewekwa katika kipengele kimoja na msanii wa kizungu.

Wakati huo huo Bieber amekuwa miongoni kati ya wasanii watakaoshindwa kuhudhuria sherehe hizo kutokana na madai kuwa amepanga kwenda sehemu wiki ambayo tuzo hizo zitafanyika huku akiongeza kuwa hadhani kama tuzo za Grammy ni muhimu hasa linapokuja suala la waimbaji vijana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents