Burudani

Drake avunja show yake ya Amsterdam baada ya kuugua ghafla

Drake amelazimika kuvunja show yake aliyotakiwa kufanya katika ukumbi wa Ziggo Dome mjini Amsterdam, Uholanzi Jumatatu hii.

Imedaiwa sababu ya rapper huyo kuvunja show hiyo ni baada ya kuugua ghafla ndipo madaktari wake walipomtaka kupumzika kwa muda. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mmoja wa washereheshaji wa kike katika ukumbi huo wenye uwezo wa kuchukua wa 170,000, Drake atatumbuiza tena Jumatano hii katika ukumbi huo.

“I’m really sorry to tell you that tonight’s show cannot take place. Drake got sick. His doctor told him not to perform. Tickets will stay valid for the show on Wednesday as he wishes to bring his fans the best show in the world,” amesema mshereheshaji huyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents