Burudani

Dr. Dre apigwa pingu na kushikiliwa na polisi kwa kudaiwa kumtishia mtu na bunduki

Rapper na producer mkongwe nchini Marekani, Dr. Dre alikamatwa na kupigwa pingu na polisi baada ya mtu mmoja kudai kuwa alimtishia na bunduki, mtandao wa Page Six umeripoti.

520022374

Mkuu wa Polisi wa Los Angeles alidai kuwa mtu huyo aliwaeleza kuwa alikuwa ameegesha gari nje ya nyumba ya Malibu, Calif. ndipo Dre akamtaka aondoke na kumwonesha bunduki.

Dre, ambaye jina lake halisi ni Andre Young, aliwaeleza polisi kuwa hakuwa na bunduki na kwamba mtu huyo alikuwa ameziba njia. Amedai kuwa mtu huyo aliondoka baada ya Dre kumchukua video.

Dre alipigwa pingu kwa muda wakati akihojiwa. Hakuna silaha iliyopatikana kwenye eneo la tukio.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents