Habari

Donald Trump kutoza 20% ya bidhaa za Mexico kwa ajili ya ujenzi wa ukuta

Baada ya Rais wa Mexico, Enrique Peña Nieto kuweka wazi kuwa nchi yake haitachangia ujenzi wa ukuta kati yake na Marekani, Rais Donald Trump amebuni njia mpya ya kupata fedha za ujenzi huo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotoka Alhamisi hii kutoka katika ikulu ya Marekani,  Rais Trump anaweza akatoza asilimia 20 ya kodi ya bidhaa zote zinazoingizwa nchini humo kutokea Mexico ili kuwezesha mpango wake wa ujenzi wa ukuta huo.

Awali Trump alipendekeza kuwa sehemu ya dola bilioni 25 wanazopewa wahamiaji kila mwaka zitumike kujengea ukuta huo, jambo ambalo Mexico imepingana nalo.

Hata hivyo mmoja wa watu wa Rais Nieto, Vicente Fox amesema iwapo Donald Trump atatimiza dhumuni lake hilo la kutoza kodi bidhaa za Mexico ana imani Mexico nayo italipiza jambo hilo kwa kutoza kodi bidhaa za Marekani zinazoingia nchini humo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents