Burudani

Dogo Janja azungumzia kijacho baada ya kutoka Mtanashati

Rapper kutoka Arusha, Dogo Janja amesema changamoto alizokutana nazo katika maisha yake tangu ameanza muziki mpaka sasa zimemfanya aitambue vizuri zaidi tasnia hiyo.

janja

Dogo Janja ameiambia Bongo5 kuwa kwa sasa anaweza kufanya kitu chochote hata akiwa mwenyewe kwa kuwa muziki umemlea na amekua nao.

“Mkataba wangu umeisha safi na Ostaz Juma,kila mtu yupo kiroho safi na mwenzake,mimi kwa sasa nipo solo artist lakini najua naenda wapi kwa sasa. Mimi hapa ni msanii ambaye nimeshakuwa na mimi kama mimi naweza nikasema muziki umenilea. Mimi nimekulia kwenye huu muziki naelewa changamoto zake na matatizo yake,kwanza nakuwa nausoma huu muziki na naulewa huu muziki unavyokwenda. Sasa nipo solo artist na ninaweza kujiunga na kundi lolote,team yangu ya taifa ni watoto wa bibi ,nipo tayari kujiunga na kundi lolote lakini itakuwa kwa mikataba maalum,” amesema.

Dogo Janja amesema yapo makundi ya Arusha yanayomsaidia mpaka atakaposimama vizuri.

“Mtaani kwetu kuna kitu kinaitwa ‘Watoto Wa Bibi’ haw watoto wa bibi kuna Jambo Squad, kuna Maker Cheka,kuna Dogo Janja na wengine mengi haya ni makundi tofauti lakini vipo katika sehemu moja. Tunasaidiana kwa namna moja hama nyingine mpaka pale mtu ambapo anakuwa amesimama vizurI.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents