Burudani

Dogo Janja akitaja kikwazo cha muziki wa Bongo

Rapper Dogo Janja amesema kiu ya wasanii hapa nchini kwa serikali ijayo ni kuona wanapatiwa haki miliki ya kazi zao.

Dogo Janja

Dogo Janja ameiambia Bongo5 kuwa maisha mabaya kwa wasanii yamesababishwa na mfumo wa sanaa wa Tanzania ambao hauwanufaishi wasanii.

“Sioni kama ina maana kila mtu tumuulize wewe upo upande gani? Au wewe unamsapoti nani? Kila mtu ana haki ya kuchagua chama anachotaka. Kikwete kiukweli amecheza nafasi yake kwa wasanii, tuongee ukweli. Japo kuna mambo ya msingi bado kama sheria ya haki miliki,” amesema.

“Lakini haya tunayakabidhi kwa serikali ijayo. Sisi wasanii tatizo letu ni haki miliki. Shida ya wasanii ni haki miliki. Tukifanikiwa kupewa haki yetu kwa tunachofanya, basi wasanii tutafika mbali sana,” aliongeza rapper huyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents