Burudani

Dj Khaled awataja mastaa wengine aliowakutanisha kwenye albamu yake ‘Major Key’

Baada ya siku chache kuthibitisha kumweka Jay Z na Future kwenye albamu yake, Dj Khaled amewaongeza mastaa wengine waliokuwa ndani ya albamu hiyo.

1-Zdt2NFm07C9CvZJ_yGF4LQ

‘Mojor Key’ ni albamu ya kwanza kwa Dj Khaled akiwa chini ya menejimenti ya Rock Nation inayomilikiwa na Jay Z.

Akiongea na EW, Dj Khaled amewataja Lil Wayne, Drake, Rick Ross, Big Sean, Chris Brown, August Alsina na Travis Scott ni wasanii ambao amewashirikisha kwenye albamu hiyo ambayo inatarajiwa kutoka mwaka huu japo haijatajwa ni lini itatoka. Lakini ameongeza kuwa bosi wake, Jay Z ana verse mbili zilizofunga albamu hiyo.

Mkali huyo kwa sasa bado anazunguka na Queen Bey kwenye ziara ya Formation.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents