Burudani

Dj Khaled anunua jumba la kifahari kwa zaidi ya shilingi bilioni 20

Dj Khaled ameuanza mwaka kwa kuonesha jeuri ya fedha. Amenunua jumba la kifahari lenye thamani ya dola milioni 10 ambapo kwa fedha za kitanzania ni zaidi ya shilingi bilioni 20.

Kwa mujibu wa mtandao wa Variety, nyumba hiyo ambayo ipo katika eneo la Beverly Hills ilikuwa inamilikiwa na muimbaji wa Pop wa Uingereza, Robbie Williams ambayo aliinunua mwaka 2002 kwa kiasi cha dola milioni 5.45.

Nyumba hiyo ina vyumba 7 vya kulala, mabafu 11, bwawa la kuogelea, sehemu ya mazoezi na vitu vingine.

“I told my son ASAHD not only will you have the house in Mia on water I’m buy u 4 mansions aka estates in diff cites ASAHD everyTING for you,” ameandika Dj Khaled kwenye mtandao wake wa Twitter. Tazama hapa chini picha zaidi za nyumba hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents