Burudani

Diva: Uwazi waniombe radhi kwa habari yao iliyosababisha usumbufu mkubwa kwa familia

Leo gazeti la udaku la Uwazi katika ukurasa wake wa kwanza limeandika habari isemayo, ‘Zitto Kabwe akiwa Rais 2015: Nani First Lady?

Katika habari hiyo, Uwazi imewataja mastaa kadhaa ambao linahisi wanaweza kuwa wake wa mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini aliyeonesha nia ya kugombea urais mwaka 2015.

Mastaa hao ni pamoja na Wema Sepetu, Jackline Wolper, Jokate Mwegelo, Lisa Jensen, Rose Ndauka, Flaviana Matata na Loveness aka Diva.

Uwazi limeandika, “Mwenyewe (Zitto) ashindwa kujibu, warembo wote wachambuliwa, sasa Zitto ataamua kusuka ama kunyoa.”

Habari hiyo imemkera Diva ambaye amesema imeanza kumletea shida kwa familia yake na kulitaka Uwazi limuombe radhi.

“Think writer wa Uwazi la Leo shuld ow me an Apology kiukweli. Umenisababishia usumbufu mkubwa sana kutoka kwa family& friends,” ametweet.

“Being first lady of the nation, doesn’t really interest me.at all …. so the first lady bullshit it has to stop. Sitaki&sipendi.”

Bado watu wengine walioandikwa kwenye habari hiyo hawajasema lolote.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents