Burudani

Ditto: Sikutarajia kupata heshima niliyoipata kwenye ‘Moyo Sukuma Damu’

Hitmaker wa ‘Moyo Sukuma Damu’ Ditto amefunguka kuwa hakutarajia kuona heshima inayoupata wimbo wake huo hivi sasa.

Ditto ameiambia Bongo5, “Ukifanya kazi unatarajia unafanya kazi nzuri lakini kiwango cha namna watu watu wanapokea sidhani kama yupo mtu anaweza akakadiria ni namna gani watu watapokea ile kazi. Siwezi kusema nilitarajia kama itapokelea hivi lakini nilijua nimefanya kazi nzuri na watu watasipenda.”

“Reaction ya watu wanaponiona kwanza, unajua sisi artist unatoka unaenda kwenye interview kituo fulani kikubwa cha redio ukifika hata ile reaction ya watangazaji wakikuona unaona kabisa ule wimbo umewashika kwa kiasi kikubwa, ukifika mlangoni hata kama ni walinzi watasema njoo tupige picha kwanza .”

Muimbaji huyo ameongeza kuwa amekuwa akipokea simu nyingi za wasanii mbalimbali wakiwemo wa Bongo na Kenya wakitaka kufanya naye kazi nao ya kuwaandikia nyimbo, kushiriki kwenye chorous ya nyimbo zao au kufanya remix ya ‘Moyo Sukuma Damu’.”

Mpaka sasa wimbo huo umeshatazamwa mara 742,557 kwenye mtandao wa YouTube.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents