Burudani

Ditto aeleza kwanini anaishi na mpenzi wake kwa miaka 5 bila kufunga ndoa

Muimbaji na mtunzi wa nyimbo, Lameck Ditto ambaye ni baba wa mtoto mmoja amesema muda haujafika wakufunga ndoa na mpenzi wake aliyedumu naye kwenye mahusiano kwa miaka 5.
ditto2

Ditto amesema kukaa muda mrefu kwenye mahusiano na mpenzi wake huyo bila kufunga ndoa ni utaratibu ambao wamejipangia wenyewe kwenye maisha yao.

“Kwa sasa na mtoto mmoja ambaye naishi naye pamoja na mama yake,” Ditto alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV. “Bado hatujafunga ndoa lakini tumshukuru Mungu huu ni mwaka wa tano tupo pamoja. Suala la ndoa naweza kusema bado ila muda wowote tufanya hivyo kwa sababu suala la ndoa ni mpango wa watu wawili, kwahiyo sisi tunaishi vizuri kwa muda mrefu kama kufunga ndoa ni kuhalilisha tu,”

Pia muiambaji huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwa ajili kazi zake mpya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents