Burudani

Director Enos Olik wa Kenya azungumzia kuhusu wasanii kushoot video SA, na baadhi ya video kutoka EA kutochezwa Trace na MTV Base

Enos Olik ni muongozaji na mtayarishaji wa video za muziki kutoka Kenya, ambaye ameshafanya kazi na wasanii wengi wa Afrika kuanzia A-list hadi wale wa kawaida.

enos-2

Shaa, Young Dee, Alikiba na Christian Bella ni baadhi ya wasanii wa Bongo ambao wameshampa ulaji director huyo kufanya video zao. Video zingine alizofanya ni ‘Kioo’ ya Jaguar, ‘Sura Yako remix’ ya Sauti Sol na Iyanya, ‘Never Been Loved’ ya Maurice Kirya, ‘Touch Me There’ ya Redsan ft. Nyla na zingine kadhaa wa kadhaa.

enos4

Bongo5 imefanya mahojiano mafupi na Enos Olik ambaye amejibu maswali matano kama ifuatavyo;

Recently kumekuwa na ongezeko la wasanii wengi wa East Africa kwenda kushoot video na directors wa South Africa, upande wako ukiwa miongoni mwa the best directors wa EA what is your point of view about this?

Enos: I personally like south Africa as a location Inazo scenes different na za EA. Kuhusu wasanii kwenda huko, i believe kila mmoja ako na vision wakati anapotoa ngoma na depending on this and budget wanaeza amua ni director yupi anafaa. Kama video shoot Ipo SA then it makes sense kutumia director wa huko juu wanaelewa the place better. the same artists pia wakishoot video EA huwa majority wanatumia directors wa EA.so it’s all balanced out.

Tumeshaona videos zako nyingi zikichezwa channels kubwa kama Trace na MTV, hapa Tanzania kuna directors wazuri pia ambao wanafanya kazi nzuri lakini video zao hazipati nafasi ya kuchezwa na channels hizo japo wasanii husika wanasema wanazituma, unawashauri wafanye nini ili video zao zipate nafasi ya kuchezwa huko?

Enos: Generally there’s a big notion kuwa video yako ikichezwa kwenye stations za nje, it’s a good video, lakini ukweli ni not all good videos make it to these stations. Wasanii lazima watambue hizi stations zipo na criteria ambazo wanatumia ku decide if videos zitachezwa au la..from the artist’s brand, quality ya song na finally quality ya video..so video inaweza kuwa nzuri but song haiko poa, so it has to balance..nawashauri washughulike kufanya clips nzuri bila ya kujali kama itachezwa kwenye hizo stations au la..at the end of the day i believe product kizuri will sell itself..that’s from artist, ngoma na video.

Kuna watu wanasema East Afrika tumebarikiwa kuwa na locations nyingi nzuri ambazo wasanii wetu bado hawajazitumia, do you agree? Any advice?

Enos: East Africa has some of the best sceneries in Africa. Kwa mfano on your way to arusha from Namanga, scenery unayopitia ya barabara na backdrop ya mount Kilimanjaro ni amazing and breathtaking. Hapa kenya, tuna beaches, highlands and landscapes. Already Nigerian directors and artists wanasafiri huku kushoot clips zao, kwa mfano ‘laye’ by ‘kiss daniel’ was shot in Mombasa, Kenya. Same pia na uganda. It’s only time a matter of time before the trend catches on lakini wasanii wetu lazima wasaidie kumarket EA. to create the trend na eventually artists from the rest of the continent will notice and rush kufanya clips zao East Africa.

Director gani wa Tanzania unayemkubali zaidi kwa sasa? And why?

Enos: Tz Hanscana anafanya vizuri. why?, apart from him kuwa rafiki yangu, amekuwa consistent kutoka creative and quality music videos. Pia kuna directors wengine TZ wanafanya vyema na i see clips zao time to time.

Msanii gani wa Tanzania unayetegemea kushoot naye video hivi karibuni?

Enos: Nimefanya kazi na Bella na Ali Kiba, kuna wengine tuko katika harakati ya kazi.

Historia ya Olik inaonesha kuwa kabla ya kuwa music video director, alianza kama msanii, baadaye akawa mpiga picha za kawaida na hatimaye akaingia kwenye utengenezaji wa video za muziki, kazi anayoendelea kufanya hadi sasa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents