Michezo

Dimitri Payet agomea mazoezi ya West Ham, anataka aondoke

Kocha wa klabu ya West Ham Slaven Bilic amesema kuwa mshambuliaji Dimitri Payet amekataa tena kuichezea West Ham, lakini klabu hiyo haiko tayari kumuuza.

Raia huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 29 amekuwa akihusishwa na suala la kuihama timu hiyo.

”Tumesema kuwa hatuwezi kuwauza wachezaji wetu wazuri lakini Payet hataki kutuchezea tena”, alisema Bilic.

”Hatuwezi kumuuza”. Payet alijiunga na West Ham kutoka Merseille kwa kitita cha pauni milioni 10.7 mnamo mwezi Juni 2015.

Alifanikiwa katika msimu wa kwanza na klabu hiyo ,akifunga mabao 12 na kuteuliwa miongoni mwa tuzo la wachezaji bora la kila mwaka.

Hadi sasa hivi ameshafunga magoli matano katika msimu huu, Payet ameshindwa kufikia kiwango kama hicho na gazeti la The Sun liliripoti wiki ilioipita kwamba Bilic alimuagiza mchezaji huyo kubadili tabia yake.

Aliachwa nje katika mechi ya FA siku ya Ijumaa ambapo West Ham ilifungwa 5-0 na Manchester City.

West Ham iko nafasi ya 13 katika ligi ya Uingereza, alama saba juu ya eneo la kushushwa daraja na sasa itakutana na Crystal Palace siku ya Jumamosi. Payet anayepokea mshahara wa pauni 125, 000 kwa wiki ameonyesha nia ya kutaka kuachana na West Ham United ambayo msimu huu imeshindwa kuonyesha cheche.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents