Michezo

Diego Costa apata jeraha la pua mazoezini

Meneja wa Chelsea Guus Hiddink amesema kwamba mshambuliaji wa klabu hiyo Diego Costa aliumia puani akiwa mazoezi jana jioni.
Hata hivyo, Mholanzi huyo amesema Costa hayumo hatarini na anatarajiwa kuwepo katika mchezo wa leo Jumamosi dhidi ya Newcastle.

3123D3F200000578-0-image-m-27_1455308859720

Hiddink amesema Costa aliumia kimakosa akijaribu kupiga mpira wa kichwa.

Kuhusu beki wa Ufaransa Kurt Zouma, Hiddink amesema mchezaji huyo hataweza kucheza tena msimu huu baada ya kuumia kwenye goti wakati wa mechi dhidi ya Manchester United.
Hata hivyo, amesema klabu hiyo itatumia wachezaji chipukizi kuziba pengo atakaloacha.

“Hatuna wasiwasi wa kuingiza chipukizi,” amesema.
Hiddink amesema klabu hiyo sasa imefanikiwa kuondoa wasiwasi na kutojiamini lakini sasa lazima wachezaji hao waanze kushinda mechi.

Chelsea hadi sasa wametoka sare mechi sita kati ya nane walizocheza tangu Hiddink achukue timu hiyo kufuatia kufutwa kwa Jose Mourinho mwezi Desemba.
Hata hivyo, hawajashindwa mechi hata moja.
“Ingawa ni vyema kutoshindwa, kila mtu sasa anataka tushinde mechi nyingi,” amesema Hiddink

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents