Michezo

Diego Costa aachwa kwenye kikosi cha Chelsea kitakachochuana na Leicester City

Kinara wa mabao katika ligi kuu ya England na mshambuliaji wa Chelsea, Diego Costa ameachwa katika kikosi kitakachomenyana na Leicester City weekend hii kwa kile kinachoelezwa kupishana na kocha wa timu hiyo Antonio Conte.

Inaelezwa katikati ya wiki hii Costa alipata ofa kutoka China inatakayomfanya kupokea kitita cha pauni milioni 30 kwa mwaka,mshahara ambao ungemfanya kua mmoja kati ya wachezaji ghali ulimwenguni.

Ofa hiyo ilimfanya Diego Costa kushindwa kuwa katika hali yake ya kawaida na kushindwa kufanya mazoezi na wenzie kama ilivyo ada,jambo liliomchukiza kocha wa timu hiyo Conte ambaye inasemekana alisikika akibwatuka ‘Nenda China.’

Hii ni habari mbaya kwa Chelsea,kwani Diego Costa amehusika kwa kiasi kikubwa kuiweka kileleni mwa msimamo kwa kuchangia magoli 19 ambapo amefunga 14,ameasist 5.

By Eliezer Gibson greencitynative

Instagram: @gibson_elly

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents