Habari

Diddy anunua na kuhamia kwenye nyumba ya thamani ya shilingi bilioni 66!

Diddy anahamia kwenye maeneo ya watu wazito jijini Los Angeles.

image

Mtandao wa TMZ umedai kuwa staa huyo amenunua nyumba katika maeneo hayo yenye thamani ya dola milioni 40 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 66. Ipo maeneo ya Holmby Hills karibu na eneo alilofariki Michael Jackson.

Nyumba hiyo ina vyumba vinane vya kulala na mabafu 11. Ipo kwenye eneo la futi za mraba 17,000 ikiwa na eneo jingine la nje lenye futi za mraba 3,000.

Pia nyumba hiyo ni mpya kabisa kwakuwa imejengwa miezi sita tu iliyopita.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents