BurudaniDiamond Platnumz

Diamond: Sina mpango wa kufanya album, hazilipi

Diamond Platnumz hana mpango wa kutoa album kwakuwa anaona ni biashara isiyo na faida kwake.

Diamond-alipanda-na-gwanda-za-jeshi (1)

Alielezea msimamo wake huo wakati akihojiwa kwenye kipindi cha The Sporah Show.

“Tatizo la album kiukweli kabisa nyumbani album inakuwa haziuziki sana. Unajikuta unaweza ukatoa nyimbo zako kumi au nyimbo nane zote zikawa ziko mtaani halafu hakuna hela uliyopata. Yaani inawezekana hela unayopata haifikii hata hela unayopata kwenye show,” alisema.

“So kibiashara ya muziki kwangu mimi nahisi imenifelisha na inanitia umaskini kwa sababu ninaokoa nyimbo nyingine nikizihifadhi nikatoa mwakani au mwaka kesho kutwa. Kwasababu nyimbo nane kama ni mfanyabiasha mzuri wa muziki unaweza kuzitoa ndani ya miaka miwili au mitatu hata minne. Ninaweza nikajipa uhai mrefu wa maisha yangu ya muziki kuliko nikitoa album ambayo haiuzi inakuwa na faida gani?”

“Ndio naonaga bora nisifanye kwa sababu kiukweli album hazilipi, labda utatapa pesa kwenye caller tune.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents