Burudani
Diamond Platnumz kutumbuiza Toronto, Canada Jumamosi Ijayo
Diamond Platnumz ni miongoni mwa wasanii wa Afrika wenye ratiba ngumu sana kwa sasa, kutokana na mfululizo wa show za nje na ndani ambazo anaendelea kuzifanya.
Baada ya weekend iliyopita kutumbuiza kwenye show ya ‘Africa Unplugged’ jijini London akiwa na Davido na Tiwa Savage, mwimbaji huyo wa ‘Mdogo mdogo’ ambaye bado yuko Uingereza Ijumaa (September 19) atakuwa na show nyingine London, Jumamosi (September 20) atakuwa Stuttgart, Ujerumani na Jumamosi ya wiki Ijayo (September 27) Diamond na kundi lake la Wasafi watakinukisha Toronto, Canada.