Burudani

Diamond na Alikiba: Sisi hatuna beef jamani! (Video & Audio)

Get a life guys, Diamond na Alikiba hawana beef yoyote… at least kutoka kwa kauli zao wenyewe.

ALIKIBA55

Superstars hawa wa Tanzania weekend na wiki hii walikuwa na interview kwenye vyombo tofauti vya habari na kuulizwa swali linalofanana,” mna beef?”

“Beef hakuna, mimi sidhani kama kuna hiyo kitu,” Alikiba aliambia One on One ya Citizen TV Ijumaa iliyopita.

“Sisi ni wasanii kuna watu wanatuangalia, then tuko na fans, Diamond ana fans wake, mimi nipo na fans wangu. Sometimes they do it for fun you know that’s what I know from my opinion. Mimi na Diamond hatujawahi kukutana sehemu tukagombana tukasemeana hivi,” alisema Kiba.

“Vile vile kitu ambacho sipendi ni mimi kufananishwa na Diamond. Mimi nafanya muziki wangu ambapo hakuna mtu anaweza kufanya muziki wangu sababu kila mtu ana talent yake and I believe I am versatile, nin hicho kipaji cha kubadilika kila wakati. So kama Diamond yuko interested kufanya featuring na watu wengine mimi nafanya muziki ninaotaka mimi na yeye anafanya wa kwake kila mtu ana style yake ya ufanyaji muziki,” aliongeza.

Kwa upande wa Diamond jana alihojiwa kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM alikokutana na swali hilo hilo.

“Sijawahi kuwa na beef nae hata siku moja, “ alijibu wa ufupi.
Kwa upande wa mtazamo wake kuhusiana na timu zao, staa huyo alisema, “ Sioni kama kuna ubaya wowote, kila mtu ana maamuzi kumchagua mtu anayemtaka yeye kumshabikia, huwezi kumlazimisha mtu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents