Burudani

Diamond aungana na Mafikizolo kurekodi wimbo uitwao Tell Every One wa kampeni ya ‘The Global Goals’

Fresh kutoka kurekodi wimbo na Ne-Yo, Diamond Platnumz amekwea pipa kutoka Nairobi kwenda nchini Afrika Kusini kuungana na Mafikizolo kurekodi wimbo uitwao ‘Tell Every One’ ambao ni sehemu ya kampeni ya dunia ya kutokomeza umaskini, maradhi, njaa na matatizo mengine, The Global Goals.

11373888_852445964863527_348235188_n
Diamond akiwa studio jijini Johannesburg kuandika na kurekodi sehemu ya wimbo huo

Mafikizolo tayari wameshaingiza sauti zao na aliyekuwa anakisubiriwa ni Diamond ambaye huenda leo akamaliza sehemu yake.

Studio Joburg South Africa Muda huu nikirecord nyimbo kwajili ya kutokomeza Umasikini Africa…. #TellEveryone #SustainableDevelopment @TheGlobalGoals,” ameandika Diamond kwenye picha aliyoweka Instagram.

Mchezaji wa Real Madrid, Gareth Bale naye ni sehemu ya mastaa duniani waliopo kwenye kampeni hiyo.

“On September 25th 2015, 193 world leaders will commit to 17 Global Goals to achieve 3 extraordinary things in the next 15 years. End extreme poverty. Fight inequality & injustice. Fix climate change. The Global Goals for sustainable development could get these things done. In all countries. For all people,” yanasomeka maelezo kwenye tovuti ya Global Goals.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents