Burudani

Diamond: Kuna msikiti ninaujenga Mtwara

By  | 

Diamond amejitolea kujenga msikiti.

Hitmaker huyo wa ‘Marry You’ amesema kwa sasa anajenga msikiti huo lakini upo mkoani Mtwara.

“Mimi nakushukuru sana mama yangu, asante sana. Naamini kabisa nitakuja Mtwara, Mtwara kule sasa hivi kuna msikiti ninaujenga na inshallah nikimaliza nitaenda kuuzindua,” alisema Diamond Jumamosi iliyopita kwenye sherehe ya 40 ya mtoto wake Nillan iliyofanyika nyumbani kwake Madale.

Diamond alisema maneno hayo wakati akimshukuru mama mmoja ambaye alimkabidhi viwanja viwili vya hekta 17 kwa kila kimoja huku kimoja kikiwa ni kitalu cha gypsum.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments