BurudaniDiamond Platnumz

Diamond kuachia video za ‘Mdogo Mdogo’ na ‘Bum Bum ft. Iyanya’ kwa pamoja Jumatatu ijayo, pia ijue sababu ya yeye kutopanda jukwaani baada ya Davido kuchukua tuzo ya BET

Jumatatu Ijayo vituo vya runinga vya Afrika vitapokea video mbili mpya za mshindi wa tuzo 7 za KTMA Diamond Platnumz. Kama ambavyo Diamond tayari ameelezea mipango yake ya kutoa nyimbo mbili kwaajili ya masoko mawili tofauti, video moja ni kwaajili ya vituo vya nyumbani Tanzania na Afrika Mashariki, na ya pili ni kwaajili ya vituo vya Afrika magharibi.

diamond

Meneja wa Diamond, Babu Tale amesema video ya ‘Mdogo mdogo’ ambayo tayari audio imetoka itakuwa kwaajili ya TV za Tanzania na ‘Bum bum’ aliyomshirikisha Iyanya wa Nigeria itakuwa kwaajili ya TV za Afrika magharibi.

“Next week Monday tunaachia video mbili kwa wakati mmoja, tunaachia nyimbo ya mdogo mdogo kwa ajili ya African market especially East africa na Tanzania, tunaachia Bum Bum kwaajili ya west market”. Amesema Tale kupitia XXL ya Clouds FM leo.

Kuhusu kwanini Diamond hakupanda jukwaani baada ya Davido kushinda tuzo ya BET na kuwaomba nominees wenzake wa kipengele cha ‘Best Insternational Act: Africa’ ambacho Diamond alikuwa akiwania pia, wapande nae jukwaani, Tale ametoa sababu:

“Zile Tuzo zinarekodiwa before, diamond alikuwa anajua zile tuzo zinakwenda Live, sababu wote hawakuwa wameambiwa zinakwenda live au zinarekodiwa, wote wamelala kwenye hotel moja LA. Wakati wao wanamgongea Davido chumbani kwake alikuwa yuko tayari, Diamond alikuwa anajiandaa jioni ndo anakwenda kwenye hiyo show ya BET. Mwisho wa siku kwasababu wale walikuwa wanaenda na ratiba wakaona tutachelewa….hakujua kama inarekodiwa na wala hakujua kama Davido amechukua tuzo mpaka mimi ndio niliyemwambia”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents