BurudaniDiamond Platnumz
Diamond kuachia video mpya wiki hii, vipi kuhusu rangi nyekundu?
Diamond Platnumz anatarajia kuachia video ya wimbo wake mpya wiki hii.
Ametangaza habari hiyo kupitia Twitter.
Kaa karibu na Social Media na Tv zako… Ndani ya Wiki Hii Nakudondoshea Video Mpya…?? #SimbaKasema
— Chibu Dangote (@diamondplatnumz) February 9, 2016
Hajasema ni video ya wimbo upi lakini kuna uwezekano mkubwa ikawa ni video ya wimbo aliofanya na AKA mwishoni mwaka jana. Video ya wimbo huo ilifanyika nchini Afrika Kusini.
Wakati huo huo Diamond na mashabiki wake wote wa WCB wamebadilisha profile picture zao na kuweka rangi nyekundu. Haijulikani inamaanisha nini lakini wanatukumbusha jinsi Tidal ya Jay Z ilivyozinduliwa na mastaa wakubwa wakiwemo Nicki Minaj, Beyonce, Usher na wengine kuweka picha za rangi ya blue bahari.