BurudaniDiamond Platnumz

Diamond asimulia kilichotokea polisi, ‘Nisingeweza kukaidi amri ya dola’

Diamond Platnumz amesalimisha nguo zake za kijeshi katika kituo cha polisi Oyster Bay jijini Dar es Salaam ambako alihojiwa kwa muda Jumatano ya wiki hii.

Diamond-alipanda-na-gwanda-za-jeshi (1)

Diamond ameliambia gazeti la Mwananchi kuwa juzi alipokea wito uliomtaka afike kituoni hapo akiwa na madansa wake pamoja na nguo hizo. Alisema haikuwa rahisi kwake kutii amri ya vyombo vya dola kwani alikuwa na woga kutokana na kutokuwa na rekodi ya yoyote ya matukio ya uhalifu.

“Nisingeweza kukaidi amri ya dola, nilifika na yale mavazi na nikahojiwa kwa saa kadhaa. Nikaeleza kwamba yalikuwa yakifanana na ya jeshi na hayakuwa sare rasmi za jeshi hilo, kikubwa nilihitaji kumaliza tatizo,” alisema Diamond.

IMG_7049
Diamond akiwa na Chifu Kiumbe wakitoka kwenye kituo cha polisi cha Oyster Bay

Diamond alisema si kweli kwamba alichukuliwa dhamana na Chifu Kiumbe, ila ukweli ni kwamba alisindikizwa na mdau huyo wa sanaa nchini kama kaka yake kutokana na woga aliokuwa nao, lakini hakushikiliwa na kutakiwa kutoa dhamana yoyote.

“Awali, meneja wangu (Hamis Tale) alishikiliwa kwa muda na mimi nikatakiwa kufika na zile nguo nikiwa na dansa wangu ambao na wao walivaa pia, nilifanya hivyo na nikafika pale na kuziacha nguo baada ya taratibu zote za kisheria kukamilika,” alisema.

Diamond alijikuta akiingia kwenye matatizo na Jeshi la Wananchi (JWTZ) baada ya kupanda jukwaani Jumamosi katika onyesho la Fiesta akiwa amevalia nguo zinazofanana na sare za jeshi hilo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents