Diamond Platnumz

Diamond aonjesha picha ya video mpya na model mrembo wa kizungu!

Diamond Platnumz alipata A kwenye somo la kucheza na akili ya mashabiki wake. Siku za hivi karibuni staa huyo amekuwa akitease mashairi ya kile kinachoonekana kama wimbo wake ujao. Na sasa amewapa mashabiki wake kitu kingine.. picha inayoonekana kuwa ni video yake mpya.

10378252_833977959957353_2677925388952221456_n

Hicho ndicho kitu pekee ambacho staa huyo huwa hatua 100 mbele zaidi ya wasanii wengi katika kazi zake. Kupitia Instagram na Facebook, Diamond amepost picha akionekana akicheza muziki na model mrembo wa kizungu. Hakuna shaka kuwa hii ni video yake mpya.

“Bahari ishachafuka ndugu zangu ntafutieni mfuko nitapike,” ameandika kwenye picha hiyo.

Alishoot lini na wapi? Hilo ni swali lenye majibu ya kukisia tu. Kisio sahihi linaweza kuwa video hiyo alishoot Afrika Kusini kipindi kile kile aliposhoot video ya wimbo alioshirikishwa na msanii wa Nigeria, Waje.

Kwakuwa ameamua kuyapeleka mambo yake kisiri kwa sasa, ndio maana huenda hakupost picha yoyote kuonesha kuwa ameshoot video mpya. Lakini kwa picha hii ya sasa, huenda Diamond akatusurprise kwa mara nyingine tena!

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents