Bongo Movie

Diamond ang’atuka, Wema, Wolper, Uwoya, Joketi mchawi nani?

diamond_wema

Juzi katika kipindi cha Take One Exclusive, niliweza kupata vitu ambavyo mimi mwenyewe sikutaka kujiuliza peke yangu nikaona ni bora nivimwage utamu wote kwenye Bongo5, kama alivyoweza kuumwaga Zamaradi Mtetema katika kipindi Chake.


Kwanza msanii wa filamu na aliyekuwa miss Tanzania 2006, Wema Sepetu alikiri kwamba kwa sasa uhusiano wake na kijana Naseer Abdulll ‘ Diamond’ kwamba upo mashakani kama sio kukatika kabisa.

Mcheza movie huyo alidai kwamba anakila ya ushahidi kwamba mwanamuziki huyo anatembea na aliyekuwa mpizani wake katika umiss mwaka 2006 yaani mshindi wa pili Joketi .

jocateJoketi;

Lakini hakuuishia hapo, pia aliwapa radhi na baraka zote kwa mwenyezi mungu kwenye mapenzi yao, lakini uvumilivu ukamshinda na kutamka wazi wazi kwamba alitegemea mpenzi wake huyo angeibwa na wanawake ambao wamekuwa wakisifika pamoja kwa umalaya kama Irene na wengine lakini imekuja kuwa tofauti.

Akuacha kueleza sifa za Joketi, kwamba ni mwanamke mlokole, mwimbaji kwaya, na mwenye kujiheshim huku akimwagia sifa kibao lakini mwisho wa sifa hizo akamalizia kwakusema kumbe ni mnafiki.

Akaendelea kusema kwamba msimamo wake upo pale pale, kwamba wanawake wa Bongo, hususani Bongo movie wanapenda kujirahisisha na kujitongozesha kwa wanaume huku wakiwatangazia wenzao umalaya wakati lengo lao ni kuharibu na kujiweka wao kwa wanume hao.

Hayo ni mengi juu ya mengi aliyoongea kuhusu uhusiano wake kati ya yeye Diamond na mpizani wake wa jadi Joketi Mwegelo.

Wolper4Jack Wolper;

Upande wa pili wa shilingi akamwangukia mwanadada mwenyewe aliyemuita Jack Wolper ingawa alisema jina hilo amelisahau. Anasema mwanadada huyo amekuwa akimsakama na kumfuatafuata ingawa hakuwa na stori naye.

Sepetu alisema kwamba Jack ametoka kwao huko Uchagani ‘hukooo Arusha’, kwamba amekuja mjini ilikuutafuta umaarufu kwa nguvu na ndiyo sababu anajaribu kuulazimisha kupitia baadhi ya watu.

Hakuishia hapo, akasema kwamba ugonvi wake na huyo anayemwita Jack Wolper kwamba ni kule wa kumdhalilisha kwa kumwambia aje aigize filamu yake moja ili anunue kitanda na godoro apate makazi ya kulala.

Jambo hilo mwana wa Sepetu anasema limemuudhi sana kwakuwa yeye kazaliwa mjini na wazazi wake wote wapo hapa mjini, na hata umaarufu umemfuata na yeye hajaufuata kama ilivyokuwa kwa mwanadada huyo.

Zaidi na zaidi amesema hategemei kuongea wala kukaa kikao na mwigizaji huyo mwenyenzake, na kama ankiongea naye ni bahati sana, kwakuwa hatarajii tenaaaa!!!!…….

jokate4

Jokate Mwegelo(kushoto) akiwa na Miss Tanzania 2006,Wema Sepetu(katikati) na Lisa Jensen(kulia). Jokate alikuwa mshindi wa pili na Lisa mshindi wa tatu. ambapo sasa hivi Ligi inaendelea kwa nje kati ya Joketi Mwegelo na Wema Sepetu.. Lundenga upoooo)

IreneWolper

Huyo alikuwa Wema Sepetu, lakini kwa upande wa pili alikuwepo Irene Uwoya Mrs Ndikumana…

Yeye kwanza alikubali aliwahi kumtamkia mumewe, kwamba anamchukia sana tena kwa mdomo wake jambo ambalo linamuuma mpaka leo. Lakini anasema haya yote yalisababishwa na madada wa Bongo Movies, ambao kila siku wanatuma meseji kwa mumewe kwa kumwambia yeye ni Malaya.

Anajiuliza kwanini wasije kumfuata mwenyewe, kwakuwa wanamjua na yanini watume  ujumbe mfupi wa simu, kwenda kwa mumewe.

Amezidi kulalamika kwa kusema kwamba hao ndiyo waliosababisha ugonvi ndani ya ndoa yake, inagawa yeye anamapungufu ambayo anajaribu kuyazuia, lakini ndiyo isiwe sababu ya kwenda kumwambia mumewe……..

Hakuishia hapo… alisema kwamba wanawake wa Bongo Movie ambao mwenyew ameshuhudia kwamba wakikubali kutoa ngo.. ngoo.. ngono kwa laki moja. Na wapo wengine wanatumwa wakawaite wenzao ili wakafanye biashara hiyo kwa fedha kidogo.

Aliendelea kwa kusema kwamba wapo wanawake ambao wameingia kwenye fani, kwakuwa waje kuuza sura, nabaadaye waweze kuuza miili yao kama wanavyofanya sasa, yaani mbele ya panzia ni ma Actress lakini nyuma ya panzia wapo tofauti sana.

Yeye hakuwa na mada ya kuongea kuhusiana na Jack wolper, lakini mtangazaji si ndiyo akamtibua kwa kumwita Jack… eti alisema “Eh Jack kwa upande wako…..?” hapo ndipo ikawa balaa kwani alisema hilo jina halitaki.

Akafunguka kwa kusema kwanza yeye ndiyo alimtoa msanii huyo, kwa kumfaninisha na Pacha wake yaani ‘Ma  P Square’, jambo ambalo analikataa katakata kwamba hawafaninai kwakuwa yeye hana tabia za kinafki kama za Jack Wolper.

Irene_uwoya_2 Irene Uwoya;
wolper3 Jack Wolper;

Jamani hakutaka kuishia hapo, alisema kwamba mwanadada huyo, aliita kundi la wasanii na kuwapa kisomo kwamba yeye anatembea na mume wake mtarajiwa.

Akazidi kusema habari hizo zikaja zikajaa na hatmaye zikavuja na kuzisikia yeye mwenyewe, na ndipo akashangaa akikutana naye wanacheka wote. Lakini taarifa alizozisikia ni mbaya, wakati huyo mwanamme tayari walishaachana na Jack, hivyo kwa Irene alikuwa kama rafiki tu, na hakukuwa na Show yoyote ikiendelea.

Irene akadadavua kwa kusema wanawake wa Bongo Movie, wakikuona na mume au mchumba basi kila saaa wanajiuliza pale unapata nini hivyo watafanya kila mikakati mpaka wamchukue, na wachungulie je kipo walichokuwa wakikitaka.

Alisema sababu hiyo ndiyo wanajikuta wakitoka na mtu bule bule au kutuma Mi sms, ya uchonganishi ilimradi walete utata, wakati kabla ya mtu huyo kuwa naye wao walikuwa wakimpita.

Irene_ndoa
Moja ya picha ya Harusi kati ya Irene Uwoya na Ndikumana;

Jamani sio mimi ila yametoka kwenye midomo yao, nimewasaidia kukufikishieni huenda kwenu umeme ulikatika si unawajua TANESCO……,,,,,, By Mo Ones

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents