Diamond Platnumz

Diamond ampa shavu msanii wa ‘Barua kwa Diamond’ Meda

Jitihada za msanii wa Iringa, Meda zimezaa matunda. Msanii huyo ambaye wimbo wake ‘Barua kwa Diamond’ umepata mapokezi mazuri, amepongezwa na Diamond Platnumz ambaye ameisikia barua hiyo.

“Kiukweli simfahamu… Sijawai hata kumuona, Wala kuzungumza nae…..na sio kwasababu Eti kaniimba mimi, hapana!… ila ni userious na uzuri wa kazi aliyoifanya ndio vimenifanya nione ni vizuri kumleta kwenu hapa wadau ili kwa pamoja tumsupport naye kesho na keshokutwa afikie malengo ya kazi yake na kuwa Balozi mzuri wa nchi yetu kupitia Bongo flavour..Huyu hapa! Anaitwa MEDA kutoka IRINGA,” ameandika Diamond.

Ombi lake la kuonana na Diamond huenda likafanikiwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents