Habari

Diamond amnunulia Wema gari jipya kama zawadi ya birthday

Jumapili ya September 28 ilikuwa ni siku ya kuzaliwa mrembo aliyebeba taji la Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu. katika kusheherekea siku hiyo mpenzi wake Nasib Abdul a.k.a Diamond Platnumz alithibitisha kwa vitendo kuwa mapenzi yao bado yako imara, kwa kumnunulia zawadi ya gari jipya aina ya Nissan.

wema6

Picha ya gari hilo la rangi nyeusi iliambaatana na ujumbe mzuri ambao Diamond alimwandikia wema kupitia akaunti yake ya Instagram yenye followers 236,841.

“Nlitama nikupe vingi, wenda ingenisaidia kueleza ni kias gani napenda nikuone ukifurahi kwenye siku yako hii ya kuzaliwa…lakini tu sina uwezo huo mumy… tafadhari pokea kidogo hichi nlichojaaliwa leo….”

wema

Mwimbaji huyo wa ‘Number’ aliitumia siku hiyo ya birthday wa Wema kusafisha tetesi zilizokuwa zimesambaa kuwa huenda wakawa wameachana, hasa baada ya magazeti ya udaku kuandika kuwa anataka kumuoa Meninah. Kabla hajapost zawadi ya birthday aliandika ujumbe huu mapema asubuhi.

“Laiti kama Maneno yangelikuwa ni sumu basi amini, Penzi letu lingekuwa lishazikwa na Kuoza…Maana sjui ni kipi hakijazungumzwa…..vya furaha, Chuki, shangwe, fitina, Vita, majungu, Misukosuko na mabalaa ya kila aina….lakini siku zote tumekuwa tukipendana na kuthaminiana kama tumeanzana jana, kwakuwa tulijua si kosa lao, ni hawajui tu niwapi tulipotokea…to the world, you may be one person…But to me, you are the world, My Beautiful World…na kama kukupenda ni uwendaazimu basi ni bora Nikabaki kwenye uchizi wangu kuliko kupata Ufahamu….i may not be physically present to stand by you while you cut your cake, but you’ll be in my thoughts the whole day! Happy birthday Darling….mmeo niko nahangaika, bt i will be coming home soon….Love you mama”

wema2

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents