BurudaniDiamond Platnumz

Diamond amkamata pabaya Jokate, Jojo amshumtumu kudhalilisha wanawake

Diamond Platnumz na Jokate Mwegelo wanaweza kuwa wamegeuka paka na chui muda huu.

10570332_780964765258673_4654914933743998636_n

Picha lilianza baada ya mshindi huyo wa tuzo ya Best Live Act kwenye MTV MAMA Awards zilizofanyika Jumamosi ya July 18 jijini Durban, Afrika Kusini kupost kwenye Instagram kipande cha video kinachomwonesha Jokate akicheza kwa furaha wimbo wake ‘Mdogo Mdogo’ kwenye hafla moja. Diamond aliweka caption ya kibabe isemayo, “Mbona Bado, Mtanyooka tu.”

Kuna tafsiri nyingi ya video hiyo lakini muhimu kufahamu ni kuwa Diamond aliwahi kuwa na uhusiano na Jokate na sasa Jokate anadaiwa kuwa na uhusiano na Alikiba (tunajua Diamond na Alikiba wako vipi).. Ni hatari tupu!

Post hiyo ya Chibu iliyovutia likes 21,642 na comments 6,329, haikupokelewa vyema na Jokate.

“Tuki-support mtu ndio kama hivi matokeo yake mtu anatumia baadae kukudhalilisha. Hii video aliyo-post kwanza ni #TBT kama sijakosea mwaka jana mwishoni nilikuwa sehemu na my friends @bikira_wa_kisukuma akani-record na kumtumia @diamondplatnumz bila mimi kujua,” aliandika Jokate kwenye Instagram. Post yake imevutia likes 8,836 na comments 5,750!

“Kiukweli sijui kwanini walifanya hivyo. Nikaja kujua baadae sana na nikaona sio big deal cause kila mtu anapenda mziki na sio dhambi kucheza mziki wowote uupendao. Ila kitendo cha @diamondplatnumz kwenda kuitafuta huko ilikokuwa hii video clip na kui-post leo najiuliza maswali mengi 1, anataka ionekana kama nilikuwa nashangilia ushindi wake? Which is not bad hakuna ubaya hapo kama unaamini ushindi wake ni sifa kwa taifa ila 2, Kwanini a-post na caption ya Na Bado Mtanyooka? Ili amkomoe nani? Au kwasababu niko karibu saaana na @alikibaofficial anatafuta kutuchonganisha? Ili iweje? Mimi I believe life goes on na kila mtu ana uhuru wa kumpenda au kuwa karibu na yule apendaye na kum-support ndio maana hata mimi nimekuacha na your new life 3, Pengine ni kweli anaendeleza zile hulka zake za kudhalilisha wanaweke aliokuwa nao waonekane sio kitu just because hawako na diamond platnumz chibu dangote. Which to me is just dead wrong,” aliongeza.

“@diamondplatnumz hizi sio tabia tunazozitegemea kwa mtu anayejisema anakomboa mziki wa Tanzania sio kwa kuweka visasi na fitna zako wazi wazi hivi. Unatu fanya tukose imani nawewe zaidi na tunaogopa ku-support cause hukawi kutugeuka. Kuwa tofauti basi, onyesha mfano kwamba kweli hupendi beef unapenda mziki wa Tanzania uendelee ila kwa ulichoki-post unaonyesha wazi UNA visirani na hutaki mema unatafuta drama, kiki, vurugu unataka kila siku uwe wewe tu ambazo kiukweli mimi binafsi siziwezi utaendelea kushinda wewe tu katika hilo na sitashindana nawewe katika hilo kwasababu siwezi nawewe unajua kama ulivyoniimba mimi mpole, sinaga maneno ( ila kwenye kazi ndio nakuwa mkali kama pilipili ). Ila ungetumia busara kidogo. Just move ON kiroho safi. Naomba pia nitumie fursa hii kukupongeza kwa tuzo yako ya MTV ila @babutale hata wewe ndugu yangu? Is this how tunaendeleza so called uzalendo? Inshallah Kheri lakini yote maisha wanyonge sisi iko siku Mungu atatunyanyua.”

Katika hatua nyingine Diamond alirejea jana kutoka Afrika Kusini na mapokezi yake yalikuwa makubwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents