BurudaniDiamond Platnumz

Diamond alitaka kuahirisha kutoa video ya ‘Number 1 RMX’ baada ya material kufutika, anatoza tshs mil 32 kwa show za ndani

Diamond Platnumz alikuwa amepanga kutoitoa video ya remix ya wimbo wake My Number 1 alioshirikisha Davido baada ya muongozaji wa video hiyo, Clarence Peter kupoteza baadhi ya material muhimu.

Akiongea na kipindi cha XXL cha Clouds FM jana, staa huyo amesema awali alipotumiwa video hiyo mwezi uliopita kuona imetokaje, aliona kuna mapungufu yaliyotakiwa kurekebishwa na muongozaji huyo.

“Wakati sasa yupo kwenye marekebisho huwezi kuamini bahati mbaya material yakafutika ikanichanganya ikawa tena hawezi akaapoligise ‘unajua imetokea bahati mbaya kwahiyo video haiwezi kubadilishwa tena inabidi iwekwe vile’,” alisema Diamond.

“Nikakaa nayo ndani nikasema ‘hii video nifanyeje’ nisiitoe, niiache ama nifanya nini?. Lakini wenyewe akina Davido, akina nani wananimbia ‘ebana hii video kali sana Diamond let’s release it na nini’ kwasababu material yamefutika, I had no choice, nikakaa nayo kama wiki tatu hivi nikasema nafanyaje sasa’. Nikaa na management ikasema ‘tuiachie tu video lakini watu wajue kuna tatizo hili na hili, so kutakuwa na mapungufu kidogo kwenye video ambayo hayakuwa ndani ya uwezo wetu,” aliongeza Diamond.

Katika hatua nyingine, Diamond amesema kwa sasa ili aweze kufanya show nchini anatoza dola 20,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 32. Amesema ameamua kutoza hivyo ili kumpunguzia promoter majukumu kama ya kumlipia hoteli, chakula na vitu vingine.

Wakati huo huo Diamond amesema video ya wimbo aliomshirikisha Iyanya wa Nigeria itafanyika hivi karibuni jijini London, Uingereza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents