Burudani

Diamond afafanua sababu za kuachia wimbo ‘Acha Nikae Kimya’ uliogusia suala la Roma

Diamond Platnumz ameachia wimbo wake mpya kwa kushtukiza uitwao ‘Acha Nikae Kimya.’ Wimbo unazungumzia masuala mengi yanayotokea sasa ikiwemo hofu iliyotanda baada ya Roma na wenzie kutekwa.

Wimbo huo hata hivyo umepokelewa kwa hisia tofauti.

Hizi ni sababu zake kwanini ameamua kuuachia:

Ili Nchi ipate maendeleo inahitaji Upendo na Ushirikiano wa Wananchi na Serikali..Na Nikiwa kama Msanii, jukumu langu ni kuhakikisha natumia Hekma na busara kukemea jambo nilionalo haliko sawa ili lirekebishwe, lakini pia panapokuwa hakuna maelewano jukumu langu pia ni kupatanisha ili kwa pamoja tujenge nchi yetu kusudi wazazi wetu, watoto pamoja na familia zetu waishi kwa Upendo Amani na kufurahia nchi yetu…Na ndiomaana kwenye nyimbo nakwambia “MI NA WEWE WA TAIFA MOJA…KAMBARAGE BABA MMOJA….SASA TOFAUTI ZA NINI TUSHIKAMANE TUKAIJENGE TANZANIA”… Unatakiwa utambue kuwa kila kiongozi ni Binadamu na kama wote tujuavyo, Binadamu hatujakamilika… hivyo katika nchi yoyote lazma wakati mwingine kuna jambo linaweza likawa haliko sawa, ila sisi kama wananchi tunatakiwa tutumie Hekima na Busara kwenye kufikisha ujumbe ama hoja zetu ili viongozi walieke sawa…Busara na Hekima itafanya viongozi watuelewe kirahisi na pengine mengi tuyatakayo tutimiziwe kirahisi… mfano mzuri, juzijuzi kupitia kipindi cha Clouds360 cha clouds Tv nlipopata bahati ya kuongea na Mh Raisi nilimuomba atufungulie Mabanda ya Chipsi na Bodaboda ziruhusiwe kufanyakazi hadi asubuhi maana zilikuwa nwisho saa 4 ama 5 usiku…kwakuwa nilitumia Hekima na busara kwenye Kufikisha hoja ama Ombi langu..alikubali na tukapewa ruksa na sasa hivi maeneo mengi ya Chipsi na Bodaboda yanafanya kazi hadi usiku mnene… hivyo tusikubali tu kulishwa Sumu za kuleta ugomvi kati yetu wenyewe kwa wenyewe eti Mara Tutukane mara sijui fanyeni hiki, wakati hata baadhi ya wanaochochea mambo hayo hawaishi Tanzania wanaishi Ulaya / Marekani / kifupi nje ya nchi…ikija kutokea bahati mbaya kimenuka wao watakuwa wanakula kuku kwa mrija huko walipo…halafu sisi na familia zetu ndio tutateseka na kuhaha kunusuru roho zetu usiku kucha.. Hatutaki makelele ya Uchonganishi mitandaoni, kama mtu kweli anauchungu na nchi na kweli akisemacho anamaanisha aje, na kwa pamoja twende sehemu husika kupeleka malalamiko sio kukaa kitandani kupost kuchochea Ugomvi kumbe anatuchora na kutufanya kama sie mataahira wake, anatupeleka mara kushoto mara kulia… Akikaa pekeake anatucheka kuwa sie wajinga wake katueka mkononi…

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents