Habari

Dhamira ya serikali kuhamia Dodoma ipo palepale – Waziri Jenista

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama amesema ratiba ya kuhamia Dodoma kwa mawaziri, manaibu, makatibu wakuu na manaibu ipo pale pale.

Waziri Jenista ameyazungumza hayo kwa wanahabari Alhamis hii mjini Dodoma na kusema uamuzi uliotolewa na Rais Magufuli upo palepale.

Alisema hata Waziri Mkuu amekuwa akisisitiza ratiba ya kuhamia Dodoma kwa awamu ya kwanza Februari mwaka huu ambayo itahusisha mawaziri, manaibu mawaziri, makatibu wakuu na manaibu wao na baadhi ya watumishi wa wizara.

“Kazi yetu itakuwa ni kuangalia utekelezaji utakuwa umefikia wapi na asiyetekeleza Waziri Mkuu atatoa mwongozo,” alisema Jenista.

Julai mwaka jana, Rais Magufuli alitangaza kuhusu serikali yake kuhamia Dodoma kabla ya kumalizika kwa muhula wake wa kwanza wa miaka mitano, na tayari Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alikwisha kuhamia katika makao makuu hayo ya nchi yaliyotangazwa mwaka 1973.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akihairisha mkutano wa nne wa Bunge la 11 mwaka jana mwishoni alitoa ratiba ya serikali ya ujumla ya kuhamia Dodoma.

BY: Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents