Habari

Mo ambwaga rais wa Nigeria na kushinda tuzo ya Forbes, ‘Person Of The Year 2015’

Mwenyekiti Mtendaji wa METL, Mohammed Dewji amembwaga rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari na wengine watatu kwenye kinyang’anyiro cha tuzo za ‘Forbes Africa’s Person Of The Year 2015’ zilizotolewa jana.

12246983_1045350848843660_8510001966156339010_n

“Congratulations to Tanzanian businessman and philanthropist extraordinaire, Muhammed Dewji on being named Forbes Africa’s Person Of The Year 2015. ‪#‎FAPOY2015‬,” wameandika Forbes

Akipokea tuzo hiyo Dewji alidai kuitoa kwa vijana wa Tanzania.

12311229_1063019103729540_1978545552083464653_n

Ushindi huo unakuja baada ya hivi karibuni Forbes kutoa orodha ya watu 50 matajiri barani Afrika.

Dewji alikamata nafasi ya 21 kwenye orodha hiyo akiwa na utajiri wa dola bilioni 1.1. Dewji anaendelea kuwa tajiri namba moja nchini Tanzania.

Rostam Aziz alikamata nafasi ya 25 kwa utajiri wa dola milioni 900 huku Said Salim Bakhresa akikamata nafasi ya 36 kwa kuwa na utajiri wa dola milioni 600.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents