Michezo

Detroit Pistons yamuacha Hasheem Thabeet

Huu unaweza ukawa ndio mwisho wa Hasheem Thabeet? Timu ya Detroit Pistons iliyokuwa imemchukua Thabeet imeamua kumwacha pamoja na wachezaji wengine watatu.

Thabeet

Thabeet, ameungana na Brian Cook, na walinzi Josh Bostic na Lorenzo Brown waliopunguzwa kwenye timu hiyo.

Mchezaji huyo alisaini mkataba usiokuwa na guarantee na timu hiyo Sept. 24, baada ya kuachwa tena na Philadelphia 76ers, waliomchukua kutoka Oklahoma City Thunder Aug. 26.

Thabeet aliingia kwenye ligi hiyo mwaka 2009 kwa kuchukuliwa na Memphis Grizzlies. Kwenye msimu uliopita alicheza mechi 23 akiwa na Thunder, na kuwa na wastani wa pointi 1.2 na 1.7 rebounds katika dakika 8.3 za kila mchezo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents