Michezo

Dele Alli akumbwa na rungu la Uefa, Arsenal na Bayern Munich nazo zakumbana nalo

Shirikisho la soka barani Ulaya (Uefa) limemfungia kutocheza mechi tatu kiungo wa klabu ya Tottenham Hotspurs ya Uingereza, Dele Alli baada ya kumchezea rafu mbaya mchezaji wa KAA Gent Brecht Dejaegere mwezi uliopita.

Katika mchezo huo ambapo timu hizo zilitoka sare ya kufungana mabao 2-2 Dele alitolewa kwa kadi nyekundu. Mchezaji huyo atakosa mechi za kwanza endapo timu yake itafanikiwa kufuzu kucheza mashindano yanayoandaliwa na shirikisho hilo msimu ujao.

Wakati huo huo Arsenal imetozwa faini ya pauni 4,300 baada ya mashabiki wake kuvamia uwanja wakati walipofungwa magoli 5-1 Bayern Munich wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani wa Emirates. Nao Bayern imetozwa faini ya pauni 2,600 baada ya mashabiki wake kuchelewesha mechi hiyo kwa kurusha karatasi uwanjani.

Timu nyingine iliyoadhibiwa ni Saint-Etienne kwa kupigwa faini ya pauni 43,000 baada ya mashabiki wake kurusha chupa na fataki uwanjani wakati wa mechi yao ya ligi ya Europa dhidi ya Manchester United kwenye uwanja wa Old Trafford mwezi uliopita.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents