Habari

DC ahofia kutumbuliwa kwa kaya kukosa choo

Mkuu wa wilaya Chunya, Rehema Madusa ametoa mwezi mmoja kwa kila Kaya isiyo na choo kutozwa faini ya laki mbili wilayani humo kwa lengo la kukwepa mlipuko wa magonjwa.

Mkuu huto wa wilaya ametoa maagizo hayo Jumatano hii wakati akiwa katika ziara yake maalumu ya kuhimiza ujenzi wa vyoo katika kata ya Chokaa na Sangabi ambapo alijionea changamoto hiyo.

“Hatutokubali ugonjwa wa kipindupindu uwe chanzo cha mimi kutumbuliwa kwenye wadhifa wangu, lazima kila Kaya iwe na vyoo safi ili kuepuka kusamba kwa uchafu wakati wa mvua,” alisema Madusa.

Serikali ya awamu ya tano imekuwa ikihimiza wakuu wa wilaya wote kuwa makini na kuwahimiza wananchi wao juu ya ugonjwa huo wa kipindupindu.

BY: Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents