Burudani

D’Banj amlalamikia Diamond kwa kumzungusha kufanya collabo, Platnumz atoa sababu za kumkwepa

Muimbaji mkubwa wa Nigeria, D’Banj amemlalamikia Diamond kwa kumzungusha kufanya naye collabo.

d n d

Kokomaster amesema kuwa toka walipokutana na Diamond walizungumza na kukubaliana kufanya collabo lakini amekuwa akimpiga chenga mpaka sasa.

Star huyo ambaye aliibuka na tuzo ya ‘MAMA Evolution’ katika MTV MAMA 2015, ameongeza kuwa kabla mwaka huu haujaisha anaamini collabo hiyo itakuwa tayari imefanyika.

Diamond ametoa sababu za kuchelewa kufanya collabo na D’Banj.

“Tulikutana kule kwenye Do Agric tukafanya Cocoa na Chocolate, tukatakiwa kufanya nyimbo ya mimi na yeye lakini nikaogopa ukianza na msanii mkubwa sana itakuwa kurudi tena itakuwa tabu lazima uanze kwa ngazi kwa ngazi kwa ngazi ili kesho na kesho kutwa ukitoa nyimbo uonekane unazidi kupanda, sio unafanya nyimbo na mkubwa halafu kesho unashuka, nafikiri ndio ikawa sababu pia nyimbo yangu ya kwanza sikuweza kufanya na yeye ya kwanza.” alisema Diamond kupitia 255 ya XXL ya Clouds Fm.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents