Burudani

Dayna Nyange alipata deal ya modeling Afrika Kusini, aeleza sababu za kushindwa kuichukua licha ya kusafiri hadi huko

Miezi michache iliyopita muimbaji Dayna Nyange alipost picha mbali mbali akiwa anasafiri nje ya nchi, lakini hakuwahi kusema kama safari hiyo ilikuwa inahusu kazi yake ya muziki au matembezi binafsi.

IMG_1965

Bongo5 imemtafuta kutaka kufahamu kama tutarajie video au collabo yoyote ya kimataifa kutokana na safari hiyo.
Muimbaji huyo kutoka Morogoro amefunguka kuwa alipata deal ya kufanya modeling na kampuni ya Afrika Kusini lakini kuna vitu vilisababisha akashindwa kuichukua deal hiyo.

Dayna-2

“Kuna watu nilikuwa nategemea ningeweza kufanya nao kazi ambao walikuwa wako South Africa lakini kuna vitu vikawa vimeingilia kati walikuwa wanataka wanipe mkataba nifanye modeling na ilibidi nikakae kule kule ili niweze nikaifanye hiyo kazi yao, “ alisema Dayna.

Dayna-1

Amesema baada ya kufanya nao makubaliano ya kiasi cha pesa anazohitaji kulipwa alihitajika kwenda Afrika Kusini kwa muda kama wa miezi miwili kabla ya kupewa mkataba wa kazi hiyo, na hicho ndio kilikuwa kikwazo kwake.

“Baada ya kupata picha zangu wakawa wametamani nifanye hivyo, japo kuwa wanaonekana wako vizuri wako wana deal nzuri za matangazo wakawa wananiambia mabango , sasa shida ilikuwa ni mwanzo mimi kwenda kukaa kule halafu ukiangalia niko na mtoto nikisema nikakae kule ni lazima niwe nimejipanga vizuri niache kila kitu huku niende kule.”

“Walitaka tusaini mikataba lakini mwanzoni nilihitajika niwepo kule kwa miezi kama miwili kabla kabla ndo vitu vingine ndo vingeweza kuwa viko sawa. Lakini kitu nilichokiangalia mimi kitendo cha kutoka hapa na mtoto wangu yuko hapa halafu mimi ndo kila kitu kwa mtoto wangu, na kitendo cha kutoka hapa kwenda sehemu nyingine bila kuwa na vitu ambavyo vimekamilika kwa asilimia zote nikahofia.”

“Unajua hii ni kazi unaweza ukawa unategemea mazuri lakini yasitokee asilimia zote au yakawa asilimia zote, kitu nilichowaambia kama wakitaka iwe hivyo watumie muda wao watafakari wajipange kama watanilipa hela niliyokuwa nataka basi, na pia nilikuwa sitaki wanibane kwenye kazi yangu ya muziki.” alimaliza Dayna.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents