Burudani

Dayna Nyange achaguliwa kuwania tuzo za BAE Awards za Nigeria

Msanii wa Bongo Fleva, Dayna Nyange amechaguliwa kuwania tuzo za BAE Awards 2017 za nchini Nigeria akiwa ni msanii pekee kutoka Tanzania.

Hitmaker huyo wa Komela amechaguliwa katika vipengele viwili ikiwemo kimoja cha BEST AFRICAN ACT akichuana na Eddy Kenzo (Uganda), King Kaka (Kenya), Stoneboy (Ghana), Jah Vinci (Jamaica).

Kipengele kingine anachowania ni BEST VOCAL PERFORMANCE FEMALE kupitia wimbo wake ‘Angejua’ ambapo anawania tuzo hiyo na Aramide, Ngowari na Rocknana (wote kutoka Nigeria).

Bonyeza hapa kumpigia kura

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents