Burudani

Dayna: Nimejifunza kutosema mambo ambayo hayajakamilika

Muimbaji wa kike, Dayna, amesema kuwa amejifunza kutosema mambo ambayo bado hayajakamilika.

Bxp5N5jCUAAxwXA.jpg large

Dayna ameiambia Bongo5 kuwa kuna mambo ambayo aliyaahidi lakini bado hayajafanyika kutokana na sababu mbalimbali.

“Nina vitu vingi ambavyo nafanya na nimefanya ambavyo vingi vipo nje ya hapa. Pia nimeshaweka connection na watu wa nje na kuna watu nimeshaanza kuweka nao mawasiliano,” amesema Dayna. “Sasa hivi nilichojifunza ni kwamba sitasema mambo ambayo hayajatimia, nitasema mambo ambayo yametimia. Kama mimi kuna mambo ambayo niliyaahidi lakini hayajatimia kutokana na vitu ambavyo vipo nje ya uwezo wangu. Kwahiyo nimeona ni bora kusema kitu ambacho kipo tayari ili kuepuka kuwayumbisha watu wako,” ameongeza.

Katika hatua nyingine msanii huyo wa ‘I do’ amesema wasanii wa kike wanahitaji msaada kutoka kwa wadau muziki hapa nchini ili kuupeleka mbali zaidi muziki wao.

“Kukubwa ninachoweza kusema sisi kama watanzania na ni watoto wa kike na tumeamua kujitoa na kufanya kazi nzuri za muziki, tunahitaji support zaidi. Maana yake sisi peke yetu kwa nguvu zetu hatuwezi kufikia malengo yetu ila kuna watu ambao tunawajua wadau ambao wanaweza wakatusupport zaidi na tukafikia malengo yetu. Sina wasiwasi na mashabiki wangu kwa sababu najua ni watu ambao wamekuwa wakinisupport toka nimeanza mpaka sasa na ninawashukuru zaidi.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents