Burudani

Daxx Cruz awataja wanamitindo wa Bongo wasiofaa kwenye tasnia hiyo

Model wa Tanzania anayefanyia kazi zake nchini Afrika Kusini, Daxx Cruz amefunguka kwa kuwataja wanamitindo wa Bongo ambao wasiofaa kuwa katika tasnia hiyo.

Kupitia kipindi cha Kikaangoni kinachofanyika kila Jumatano kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV, Daxx amewataja Calisah na Hamisa Mobetto kuwa hawafai kufanya kazi hiyo.

“Calisah NO, ni mfupi, for me No, labda kwa Tanzania, unajua model siyo kuwa na six packs, akija South hapati kazi. Mario ambaye amewahi kuwa Mr. Tanzania, kwangu no,” amesema Daxx.

“Nelly ni mzuri nampa 80%….. Eligiva for now NO, zamani alikuwa okay, sa hizi yuko na familia yake, maisha yamebadilika. Hamisa Mobetto kwa Tanzania yes, but nje ya Tanzania no, labda kwa video vixen sababu ya muonekano na height yake,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents