Burudani

Davido kutumbuiza Dar November 1 kwenye ‘The Climax’ , tamasha jipya la Times FM

Mshindi wa tuzo za BET 2014 na MTV (MAMA), Davido wa Nigeria anatarajiwa kutua tena Tanzania mwishoni mwa mwezi huu, na tayari imefahamika kuwa mkali huyo atatumbuiza kwenye tamasha jipya la ‘The Climax’ litakalofanyika November 1 jijini Dar.

davido

Kwa mujibu wa tovuti ya Times Fm, Tamasha hilo limeandaliwa na kituo cha radio Times Fm na litahusisha wasanii wengine ambao watatangazwa hapo baadae.

“Paris was Great next stop!! LONDON –LAGOS-WARRI-SOUTH AFRICA-NAMIBIA-TANZANIA lego.” alithibitisha Davido kwenye Instagram.

Mara ya mwisho kwa Davido kuja Tanzania ilikuwa ni mwaka jana (2013) kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta na ndipo msanii Diamond alipata nafasi ya kufanya nae remix ya ‘Number 1’ ambayo imemfungulia milango mingi ya kimataifa ndani ya mwaka mmoja.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents