Burudani

Davido aungana na Young Thug kushoot video ya wimbo wao

Davido ameonesha yeye ni mzito – ameendelea kuwasha moto wa kufanya kazi na wasanii wa Marekani baada kukaa zaidi ya mwaka mmoja bila ya kuachia wimbo mpya.

14712309_214725075635109_5166160218962264064_n

Muimbaji huyo wa How Long amepost picha kwenye mtandao wake wa Instagram inayomuonesha akiwa na rapper wa Marekani, Young Thug wakishoot video yao.

“I just ran it up for my people’s SAKE – @thuggerthugger1 ????????,” ameandika Davido kwenye mtandao wake huo.

Mpaka sasa ndani ya miezi miwili msanii huyo ameshaachia nyimbo zake tatu ikiwemo wimbo wa ‘How Long’ aliomshirikisha Tinashe wa Marekani pamoja na EP yake ya ‘Son Of Mercy’ iliyotoka Septemba 30 ya mwaka huu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents