Burudani

Davido adaiwa kumdiss D’Banj kwenye ‘Orekelewa’

Mwaka 2017 unaonekana unaweza ukawa umeanza vibaya kwa Davido. Muimbaji huyo amedaiwa kumdiss D’Banj kwenye wimbo wa ‘Orekelewa’ alioshirikishwa na DJ Jimmy Jatt.

Japo Davido hajataja moja kwa moja jina la D’Banj katika wimbo huo lakini mashairi yake aliyoimba ndio yanadaiwa kuwa amemlenga hitmaker huyo wa Oliver Twist.

“dem dey ask say what is the koko. I tell am say owo ni koko. Him still think say na em be koko gerrarahere,” ameimba Davido katika wimbo huo. Neno ‘koko’ katika mashairi hayo ndio linasababisha watu wafikirie kuwa Davido amemmdiss D’Banj kwa kuwa hilo ni jina jingine la muimbaji huyo likifahamika zaidi kama Kokomaster.

Tazama video ya wimbo huo hapa chini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents